Monday, October 16

Majeshi ya Iraq, yasonga mbele Kirkuk

Vikosi vya majeshi ya IraqHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVikosi vya majeshi ya Iraq
Vikosi vya majeshi ya Iraq vinasonga mbele kuelekea katika maeneo yanayodhibitiwa na Wakurdi katika jimbo la Kirkuk wakati wasiwasi ukiongezeka kati ya pande mbili kuhusu mustkabali wa Kurdistan iliopo Iraq.
Televisheni ya taifa Iraq inasema vikosi vya Iraq tayari vimedhibiti sehemu kubwa ya eneo hilo.
Maafisa usalama wa Kikurd wanasema majeshi ya Iraq yanalenga kushika udhibiti kwenye eneo hilo lenye mafuta na kuliko pia na kambi ya anga ya K1q.
Serikali ya Iraq umekuwa ukiutuhumu utawala wa Kurd kutawanya wapiganaji, Kutoka chama cha kikurd cha PKK, chenye makazi yake nchini Uturuki. Madai ambayo yanakanushwa na Wakurd.
Hali ya wasiwasi imeongezeka kati ya Baghdad na Kurd wa Iraq tangu Kurd ilipopiga kura ya maoni juu ya uhguru wake.

No comments:

Post a Comment