Monday, October 16

Magari manne yagongana Barabara ya Mandela


Ajali iliyohusisha magari manne imetokea katika barabara ya Mandela na kusababisha foleni kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Ajali hiyo ambayo imetokea saa moja imehusisha lori kubwa lililobeba katapila na mengine matatu madogo yaliyokuwa yakielekea sehemu moja.
Magari hayo yote yanamilikiwa na kampuni moja ya Kaizari General Supplies Ltd.
Kwa mujibu wa mfanyakazi wa Kampuni hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema  hakuna majeruhi katika ajali hiyo.
"Haya yote ni magari ya kampuni yetu, kilichotokea ni kwamba gari dogo lililokuwa mbele lilipata pancha na kusimama ghafla, hii ya nyuma yake ilikuwa mwendokasi , dereva alipiga breki na kupoteza mwelekeo. Hapo ndipo hili lori likaja kuigonga," amesema mfanyakazi huyo.
Shuhuda wa ajali hiyo, Betson Lemgoha amesema gari dogo aina ya Rav 4  limepinduka kwa sababu lilikuwa kwenye mwendo kasi, jambo lililomfanya dereva kukosa udhibiti wa gari hilo.

No comments:

Post a Comment