Wednesday, October 11

MABALOZI WA NCHI TATU WATETA NA SAMIA IKULU

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan,  amekutana na Mabalozi kutoka nchi tatu kwa wakati tofauti ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais alianza kukutana na Balozi mpya wa Uganda nchini, Richard Kabonero, ambapo katika mazungumzo yao,  balozi huyo alizungumzia nia ya nchi yake katika kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kindugu na Tanzania.
Uhusiano huo ni ule wa kijamii, na kiuchumi ambapo tafiti za mafuta zinazoendelea katika ziwa Eyasi, mashirikiano ya sekta ya anga ili kusaidia kukuza utalii, mradi wa ujenzi ya reli ya kati na mradi wa umeme vijijini pamoja na kuanzishwa kwa jukwaa la biashara la sekta binafsi kutoka nchi husika ili kuweza kunufaika na fursa zitakazojitokeza baada ya kukamilika bomba la mafuta .
Katika mazungumzo hayo, Samia aliipongeza Uganda kwa kutafiti na kugundua mafuta kwa kutumia wataalamu wazawa ambapo alisisitiza ushirikiano wa kitaalamu na wataalamu wa Tanzania.
Samia pia amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Lucas Hernandez, ambaye alisema Cuba imeendelea kuwa rafiki mzuri wa Tanzania na kushukuru sana Tanzania kuisemea Cuba iondolewe vikwazo kwenye mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment