Kupitia akaunti zao za kijamii za Twitter, wabunge hao wameonyesha kufurahishwa na uamuzi wa Nyalandu kujiondoa CCM na kuomba kujiunga Chadema.
Nyalandu alitangaza uamuzi huo jana Jumatatu Oktoba 30,2017.
Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu ‘Profesa Jay’ amesema, “Hongera sana my brother @lazaronyalandu kwa ujasiri na kusimamia kile unachokiamini! Karibu sana kiumeni.. #speak your mind.”
Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema, “Shikamoo Nyalandu.. raha sana.”
“Mhe. Nyalandu nikukaribishe kwenye siasa za upinzani Tz! ni siasa tamu sana kwa wenye moyo mgumu! Ni ngumu sana kwa wenye moyo mwepesi,’’ ameandika Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ameandika, “Mhe. Nyalandu karibu sana Chadema. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili Taifa letu.’’
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa yeye amesema, “Katika fani ya uandishi wa habari, taarifa ya Nyalandu ingeitwa scoop. Who will be next.”
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesema, “Hongera kaka kwa kukataa kuwa sehemu ya siasa za kishamba... siasa zilizojaa migawanyiko chuki visasi na vitisho.”
Amesema, “Umechukua uamuzi mgumu lakini sahihi, umeonyesha kwamba utu na ubinadamu ni muhimu kuliko fedha na vyeo, historia yetu itakukumbuka vizuri, karibu katika mapambano ya kudai haki na usawa.”
No comments:
Post a Comment