Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Dar es Salaam imekemea wale wanaotumia mitandao ya Kijamii,kumtukana Rais na kusisitiza kuwa wanaofanya hivyo wanawakosea watanzania kwa kitendo wanachokifanya.
Akizungumza wakati wa warsha ya siku moja ya kamati ya Amani ya viongozi wa dini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCR kwa lengo la kuwaelimisha matumizi salama ya mitandao
Mweneyekiti wa Kamati hiyo, Shekh Alhad Mussa Salum amesema Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya , ufisadi, wizi na ubadhirifu katika mali za umma hivyo wanaotumia mitandao vibaya ni kuwakosea watanzania .
Katika Mkutano huo Shekh wa Mkoa , Alhad Salum amempongeza Rais John Magufuli kwa juhudi ambazo amezichukua katika kuifanya nchi kuwa maadili kwa viongozi wa Umma pamoja na wananchi.
Amesema si suala jema kwa kiongozi wa nchi kutakanwa kwenye mitandano ,kwa kufanya hivyo ni sawa na kutukanwa watanzania waliomuweka madarakani ambapo kuwa jambo hilo halikubaliki.“Simu yako ndio pepo yako na ndiyo moto wako, ukitumia vibaya bila shaka itakupeleka motoni licha ya kuwa kiongozi wa dini pamoja na waumini wako wataingia motoni ,” amesema .
Amsema wananchi wanawajibu wa kuheshimu sheria za mitandao na za nchi na kusisitiza kuwa mmomonyoko wa maadili na kuharibika kwa tabia miongoni mwa jamii kwa kiasi kikubwa, kumechangiwa na simu hizo hivyo lazima zitumike kwa utaratibu.
Aidha amesema viongozi wa dini, makanisa na misikiti wanatakiwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuwaokoa watu kwa kuwaelimisha matumizi sahihi ya mitandao.
Naye Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Joshua Mwangasa amewataka Aidha kwa upande wa viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kuhusu matumizi bora ya mitandao ya kijamii ili kuepuka kuvunja sheria ya makosa ya kimtandao kwa kuzingatia maadili na utu.
Kwa mujibu wa Mwangasa, kila mtanzania yupo kwenye hatari ya kuingia au kuingizwa kwenye makosa ya kimtandao hivyo ni vema wananchi kuwa makini kwa kukataa kusambaza jumbe zisizo na maadili au kutoa taarifa polisi kuhusu mtu anayesambaza jumbe hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba akizungumza na kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam juu matumizi ya mitandao jinsi ya kutumia viongozi wa dini katika mkutano ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Joshua Mwangasa akizungumza Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam namna ya kutumia mitandao na Jeshi la polisi linavyofanya kazi kwa wahalifu wa mitandao,jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Shekh Alhad Mussa Salum (katikati) akiwa na Katibu Kamati ya Amani , Padri John Solomon (kulia) na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba wakisiliza mada katika mkutano wa TCRA na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Sehemu ya kamati ya amani ya Mkoa wa Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment