Mrembo huyu ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Vega nchini Afrika Kusini, akizungumza naMwananchi jana Jumatano Oktoba 18,2017 jijini Dar es Salaam, alisema amelazimika kufanya hivyo akisukumwa na uzalendo na mapenzi yake katika masuala ya urembo.
Kabete aliyekuwa mshindi wa tano katika mashindano ya Miss Tanzania 2016, atashiriki fainali za mashindano ya Miss World zitakazofanyika Sanya nchini China, Novemba 18,2017.
“Nilipoombwa kwenda kuwakilisha katika mashindano nilikuwa chuoni, ilibidi nichukue muda kuamua kama naweza kushiriki au la, nilifurahi na kusema ukweli nilikuwa na hamu ya kuiwakilisha nchi yangu,” amesema.
Amesema baada ya mashindano ya Miss Tanzania mwaka jana kumalizika, alijiunga na mashindano ya Miss Africa 2016 na kufanya vizuri.
“Nimejiandaa vizuri kwa sababu tayari nina uzoefu. Nilishashiriki mashindano ya Miss Africa Nigeria 2016 nikaingia tano bora, ninaelewa mashindano ya urembo kimataifa yakoje na ilinichukua zaidi ya mwezi kujiandaa kwenda kushiriki,” amesema.
Amesema amejiandaa katika mambo mengi, ikiwemo kutengeneza makala maalumu inayoelezea maisha yake.
“Nimejiandaa katika mambo mengi ikiwemo makala inayozungumzia mazingira ambayo nimeitengenezea Pugu na Uhuru Mchanganyiko. Inahusu mazingira safi na kwa namna gani tunaweza kufanikiwa katika masuala ya usafi kama nchi,” amesema.
No comments:
Post a Comment