Mwamanga alionyesha kushangazwa na idadi ya wanufaika 252 wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu katika Kijiji cha Makuyu wilayani Mvomero.
Alihoji kwa nini idadi haijapungua tangu 2015.
“Naona idadi ya wanufaika imeendelea kuwa hiyo hiyo, hakuna hata waliokufa?”Alihoji.
Mwamanga alisema kwa sasa mpango wa kunusuru kaya maskini unanufaisha watu milioni 1.1 hapa nchini.
Akisoma taarifa hiyo, Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makuyu, Fredrick Mhini alisema mpango huo ulianza utekelezaji Julai 2015 ukiwa na wanufaika 252 na hadi sasa idadi hiyo hiyo ya wananchi imeendelea kunufaika.
Alisema kwamba katika utekelezaji wa mpango huo, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya malalamiko mengi ya wananchi wenye sifa za kuingia kwenye mpango huo lakini wamekosa nafasi.
No comments:
Post a Comment