Wizara ya ulinzi nchini Afghanistan imesema mlipuko mmoja wa mtu aliyejitoa muhanga Jumamosi nje ya Chuo cha mafunzo ya kijeshi mjini Kabul uliwaua wanafunzi wasiopungua 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Shambulizi hilo limetokea siku moja baada ya mtu huyo wa kundi la Islamic State-IS kushambulia msikiti uliojaa waislam wa dhehebu la kishia katika mji huo na kuuwa waumini 50 na kuwajeruhi darzeni wengine.
Polisi wa Afghanistan pamoja na walioshuhudia tukio hilo walisema shambulizi la Jumamosi lilitokea baada ya mjitoa muhanga aliyekuwa akitembea kwa miguu kujilipua karibu na basi dogo lililojaa wanafunzi wa jeshi.
Tukio hilo lilitokea kwenye mlango mkuu wa kuingilia kwenda kwenye chuo cha mafunzo ya jeshi cha Marshal Fahim.
Msemaji wa wizara ya ulinzi Dawlat Waziri alithibitisha idadi ya vifo na alisema watu wane wengine walijeruhiwa.
No comments:
Post a Comment