Thursday, October 19

Bi Mugabe amshtaki mfanyibiashara kwa kutomuuzia pete ya $1.35m

Zimbabwe na mkewe Grace MUgabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionZimbabwe na mkewe Grace MUgabe
Mke wa rais nchini Zimbabwe Grace Mugabe amemshtaki mfanyibiashara mmoja kwa kushindwa kumpatia pete ya almasi yenye thamani ya $1.35m kulingana na chmbo cha habari cha Herald.
Jamal Ahmed alidaiwa kumpatia pete yenye thamni ya $30,000 badala ya ile aliyoagiza.
Ni mgogoro wa hivi karibuni kuhusu pete hiyo yenye Carat 100 iliotarajiwa kuwa zawadi ya rais Mugabe kwa mkewe wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ndoa yao.
Mwaka uliopita, bwana Ahmed aliwashtaki Bi Grace Mugabe na mwanawe wa ndoa yake ya kwanza mahakamani baada ya kuchukua mali zake katika mgogoro wa pete hiyo.
Alisema katika nakala za mahakamani kwamba bi Mugabe alitaka kurudishiwa fedha zake baada ya pete hiyo ya almasi ilionunuliwa Dubai kukabidhiwa yeye baada ya kusafishwa na mtu mwengine.
Wakati aliposhindwa kulipa fedha hizo kwa akaunti moja huko Dubai, licha ya kusema kuwa fedha hizo zilitumwa kupitia benki moja ya Zimbabwe mke huyo wa rais alichukua kwa lazima nyumba zake.
Bwana Ahmed alisema kuwa alinyanyaswa, kutukanwa na kutishiwa na kuambia hawezi kuchukua hatua yoyote kwa kuwa walioshtakiwa ndio 'Zimbabwe'.
Disemba iliopita jaji mmoja alimuagiza bi Mugabe kurudisha mali hiyo.
Na sasa anamshtaki bwana Ahmed , ambaye ana kibali cha kuishi nchini Zimbabwe na biashara katika taifa hilo kwa $1.23m ili kulipa deni hilo.

No comments:

Post a Comment