Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uhispania, amesisitiza msimamo wa serikali yake, kuwa kiongozi wa Catalonia ambaye alifutrwa anaweza kuwania tena uchaguzi wa Disemmba ikiwa hatakuwa gerezani.
Alfonso Dastis alizunguamza wakati wa mkutana wa kuunga mkono umoja wa Uhispania ambao ulifanyika katika mji mkubwa zaidi huko Catalonia wa Barcelona.
Carles Puigdemont aliondolewa ofisini baada ya Madrid kulivua eneo la Catalonia usimamizi wake baada ya eneo hilo kutangaza uhuru.
Serikali kuu ya Uhispania kwa sasa imechukua udhibiti kwa idara za Catalonia
Mkuu wa mashtaka nchini Uhispania anaandaa kumfungulia mashtaka Bw. Puigdemont na maafisa wengine wa Catalonia kwa kukiuka sheria ya Uhispania.
Bw. Puigdemont anasema hatambui amri ya kutoka Madrid ambayo ilimundoa madarakani.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nadani nchini Uhispania amewaandikia polisi wote huko Catalonia akiwataka kuonyesha uzalendo kwa awamu mpya ya uongozi.
Aliwashauri polis wote ambao sasa wako chini ya udhibiti kutoka Madrid kuhusu wajibu wao wa kufuata maagizo.
No comments:
Post a Comment