Friday, October 6

AJINYONGA BAADA YA KUUA MKE WAKE

Na Mohamed Hamad-Kiteto

MKAZI wa Kijiji cha Banyibanyi mkoani Dodoma, Mussa Chisimilo (37), amejinyonga kwa shuka hadi kufa, baada ya kudaiwa  kumuua mke wake, Edna Chisimilo (26) kwa kumkata na jembe kichwani.
Tukio hilo lilitokea Kitongoji cha Mbeli wilayani Kiteto mkoani Manyara, kutokana na ugomvi wa kifamilia ambao unadaiwa kusababishwa na wivu wa mapenzi
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimana, Willison Ngolanya, aliliambia MTANZANIA kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 4, mwaka huu.
Alisema mtuhumiwa alitekeleza mauaji usiku na kutoweka, lakini alfajiri  majirani zake walikuta  mke akiwa amefariki.
Baada ya taarifa kutolewa kwa uongozi ndipo zikapatikana tena  taarifa zingine kuwa naye amejinyonga juu ya mti kwa kutumia shuka yake.
Taarifa kutoka kwa familia zinasema marehemu wameacha watoto watatu wadogo ambao wanahitaji malezi ya karibu.
Walisema mwanamume atazikwa Kitongoji cha Mbeli ya Kiteto na mwanamke alisafirishwa kwenda Kijiji cha Dongo Kiteto.
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limethibitisha kutokea tukio hilo na kudai uchunguzi unafanyika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe, alisema mwanamume huyo alimuua mke wake kwa kumkata kwa jembe kichwani.

No comments:

Post a Comment