Wednesday, October 4

ACT-Wazalendo yarukia suala la mishahara lililozungumziwa na Rais Magufuli

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu  
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais John Magufuli kusema kuwa hatoongeza mishahara kwa wafanyakazi, Chama cha ACT-Wazalendo kimelitaka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi(Tucta) kupinga msimamo huo.
Tucta imetakiwa kusimama imara kupigania haki za msingi za  wafanyakazi ikiwemo ongezeko la mishahara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema chama hicho kipo tayari kushirikiana na wafanyakazi katika kupigania haki zao.
Shaibu amesema wafanyakazi wa Tanzania hawastahili kufanyiwa hivyo na Serikali ikizingatiwa kuwa wana mchango mkubwa katika mapato ya nchi.
"Wafanyakazi ndiyo wanaochangia zaidi kuliko waajiri wao. Hilo linadhihirika hadi kwenye kitabu cha mapato ya Serikali Kuu cha mwaka 2016/2017.
“Kitabu hiki  kinaonyesha kuwa wafanyakazi walichangia jumla ya Sh3 trilioni wakati waajiri wao walichangia Sh900 milioni," amesema

Katibu huyo wa itikadi amekwenda mbele zaidi na kuonyesha kushangazwa kwake na kauli tofauti zinazotolewa na Rais Magufuli kuhusiana na suala hilo la wafanyakazi.
"Wakati wa kampeni Magufuli alijipambanua mbele ya Watanzania kuwa atasimamia maslahi ya wafanyakazi, alirudia ahadi hiyo katika siku ya wafanyakazi mwaka huu. Waziri Kairuki  pia aliliomba Bunge kuidhinisha Sh650 bilioni kwa ajili ya nyongeza hiyo."

No comments:

Post a Comment