Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ngugai akisisitiza jambo wakati wa Kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akilieleza Bunge leo mjini Dodoma kuhusu mkakati wa Serikali kukamilisha ujenzi wa nyumba elfu kumi za makazi kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambapo kati ya hizo zaidi ya elfu sita zimeshakamilika.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid (wakwanza kulia) akifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma wakati wa ziara yake .
Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe . Hawa Ghasia akichangia hoja Bungeni leo mjini Dodoma kuhusu maboresho katika sekta ya Afya hasa suala la tohara kwa wanaume ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akisisitiza jambo mara baada ya kuwasilisha muswaada wa sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 3 wa mwaka 2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment