Wednesday, September 6

Wazazi wataka uchunguzi miili iliyoopolewa shimoni

 Wakazi wa jiji la Arusha waliokusanyika kwenye
 Wakazi wa jiji la Arusha waliokusanyika kwenye nyumba ambayo ujenzi wake haujakamilika kushuhudia uopoaji wa miili ya watoto wawili kwenye shimo.Picha na Filbert Rweyemamu 


Arusha. Wazazi wa watoto Moureen David (6) na Ikram Salim (3), wakazi wa Kata ya Olasiti, Arusha waliotekwa katika siku tofauti na kubainika kuwa wamekufa wameelekeza polisi kujua utaratibu wa uchunguzi wa miili.
David Njau, baba wa Moureen aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Lucky Vincent na Salum Kassim, baba wa Ikram wanafuatilia uchunguzi wa miili ya watoto wao iliyoopolewa kwenye shimo la choo jana Septemba 5 usiku katika eneo la Mji Mpya, Mtaa wa Olkerian.
Wakati Moureen alitekwa Agosti 21 saa kumi na moja jioni, Ikram alitekwa Agosti 26, saa 12 jioni.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, David Safari ambaye yupo pamoja na familia hizo, amesema wanakwenda kuwaomba polisi wawapatie miili kwa ajili ya maziko.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo anatarajiwa kutoa tamko baadaye kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment