Friday, September 29

Watanzania wang’ara tuzo za uandishi wa sayansi Afrika

Watanzania watatu wa Tanzania wametangazwa kuwa washindi wa tuzo za uandishi wa habari za sayansi katika teknolojia za kilimo zinazotolewa na Jukwaa la Bayoteknolojia la Afrika (OFAB), hivi karibuni Munyonyo jijini Kampala Uganda.
Mashindano hayo yalihusisha washindani 20  kutoka  Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania Uganda ambapo kila nchi ilitakiwa kutoa washindi wasiopungua watatu.
Mratibu wa OFAB Tanzania, Philbert Nyindondi aliwataja waandishi hao kuwa ni Gerald Kitabu wa gazeti la The Guardian aliyeibuka na ushindi kwa upande wa magazeti na mitandaoni, Koleta Makulwa wa Radio Free Africa (RFA), Dino Mgunda wa Star TV.
Kitabu ambaye pia ni mshindi wa tuzo hiyo nchini alipata tuzo ya Dola 1,500 na simu aina ya  iPhone 7+ yenye thamani ya Dola, 1,200, huku Makulwa naye akipata tuzo hizo na Mgunda akipata Dola 1,000 and iPhone7+ yenye thamani ya Dola 1,000.
Nyinondi aliwataja majaji waliohusika katika mchakato wa kupata washindi kuwa pamoja na jaji mkuu Otula Owuor ambaye ni mhariri wa habari za sayansi kutoka Kenya, Betty Mkwasa ambaye ni mwandishi mkongwe na aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya (Tanzania) na Mark Lynas maybe ni mwanamazingira na mchambuzi wa habari kutoka Uingereza.
Wengine ni Eve Georgia ambaye ni mshauri wa maendeleo wa mtandao wa habari kutoka Namibia na Suleiman Okoth ambaye ni mtaalamu wa mawasiliano wa Taasisi ya Kilimo cha Bayoteknolojia (AATF).
Miongoni mwa vigezo vya tuzo hizo ni pamoja uelewa kuhusu Bayoteknolojia, jitihada na usahihi katyika uandishi

No comments:

Post a Comment