Monday, September 11

Wakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao

The President of Iraqi Kurdistan, Massoud Barzani, during a BBC interview
Image captionRais wa eneo la Kurdistan nchini Iraq Massoud Barzani
Rais wa eneo la Kurdistan nchini Iraq amesema kuwa eneo hilo litachora mipaka ya taifa lao siku za baaadaye ikiwa Iraq haitakubali kura ya uhuru katika kura ya maoni ambayo inatarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Massoud Barzani aliambia BBC kuwa alitaka kuafikia makubaliano na serikali ikiwa wakurdi wanataka kujitenga.
Waziri mkuu wa Iraq amekataa kura ya maoni akisema kuwa ni kinyume na sheria.
Bwana Barzani pia ameonya kuwa wakurdi watapigana na kundi lolote ambalo litajaribu kubadilsiha hali huko Kirkuk kwa nguvu.
Kurds take pictures with Kurdish flags at the Kirkuk Governorate Council building in Kirkuk, Iraq (6 April 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao
Vikosi vya Kurdi vya Peshmerga vimechukua udhibiti wa mji huo wenye utajiri wa mafuta ambao una waarabu wengi na sehemu zingine zinazodaiwa na Baghadad kwa zaidi ya miaka mitatu.
Wapiganaji wa kishia wanasema kuwa hawataruhusu mji wa kirkuk kuwa sehemu ya eneo huru la Kurdistan.
Wakurdi ndio jamii ya nne kwa ukubwa eneo la Mashariki ya Kati lakini bado hawajapa taifa.
Nchini Iraq ambapo wanachukua asilimia 15 hadi 20 ya watu milioni 37, wakurdi wamekumbwa na miongo kadha ya ukandamizaji wa serikali za kiarabu kabala ya kujietenga kufuatia vita vya Ghuba vya mwaka 1991.
Iraqi Kurdish men look at posters bearing images of Massoud Barzani and urging people to vote in the upcoming independence referendum in Irbil (7 September 2017)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao

No comments:

Post a Comment