Mbunge wa Kaunti ya Ayivu Bernard Atiku alionekana akivurumishana na mwenzake wa Manispaa ya Arua, Mr Ibrahim Abiriga, mmoja wa wabunge wanaounga mkono kuondolewa ukomo wa umri.
Alipoulizwa Atiku kuhusu ugomvi wao alisema ulitokana na Abiriga kumshutumu kuwa alikodi vijana wa kumshambulia (Abiriga) wakati wa mechi ya mpira kati ya klabu ya Onduparaka na Maroons FC iliyochezwa Luzira.
"Nilikuwa nje ya Bunge kwa ajili ya kuchukua baadhi ya nyaraka zilizokuwa kwenye gari langu ndipo nikamwona Abiriga akiwa na kikundi cha wanahabari amesimama kwenye ngazi za jingo la Bunge. Mheshimiwa (David) Abala (wa Kaunti ya Ngora) alinisimamisha kwa ajili ya kujua habari fulani. Kwa hiyo, wakati nazungumza naye, nikamsikia Abiriga akinitukana. Kisha nilipowasogelea kumuuliza alikuwa anasema nini, Abiriga alianza kunitukana kuwa mimi ni mpumbavu na mjinga," alisema.
Atiku alisema: "Yeye (Abiriga) alidai kwamba niliwakodi vijana kumtukana wakati wa mechi kati ya Onduparaka na Maroons FC, Luzira. Nilipojaribu kumweleza Abiriga kwamba mimi sikuwepo kwenye mechi hiyo ya Jumamosi, yeye alisisitiza kwamba nilikuwepo na akaanza kunishambulia. Nilimsukuma na ndipo polisi wakafika kututenganisha."
Wakati hayo yakitokea, Bunge limepanga kujadili muswada wa ukomo wa rais leo.
Naibu Spika, Jacob Oulanyah amesema alipokea taarifa kutoka kwa Mbunge mmoja akiomba kuwasilisha hoja bungeni akiipa serikali maoni kuhusu ukomo wa umri kwa mgombea urais.
No comments:
Post a Comment