Friday, September 1

Wabunge Laac waiwekea ngumu Sengerema

Makamu mwenyekiti wa kamati Laac, Abdallah

Makamu mwenyekiti wa kamati Laac, Abdallah Chikota 
Dodoma. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) imeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuandaa upya taarifa ya hesabu zake.
Laac ilikuwa ikipitia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdallah Chikota amesema
halmashauri hiyo inatakiwa kuwasilisha taarifa hiyo ofisi za Bunge kwa ajili ya uhakiki kabla ya Novemba 30.
Chikota ambaye ni mbunge wa Nanyamba amesema halmashauri hiyo imebainika kufanya makosa mengi katika utayarishaji wa taarifa ya hesabu kwa kutozingatia vigezo vya kimataifa.
“Halmashauri hii haikutenganisha hesabu za kawaida na zile za maendeleo. Mfano, Sh3.9 bilioni zilitakiwa kutolewa maelezo ya
ziada kwenye hesabu za mwaka 2015/2016 lakini hawakufanya hivyo,” amesema.
Tofauti ya madeni yaliyoainishwa kwenye taarifa iliyowasilishwa mbele ya kamati na kiasi kilichoainishwa kwenye hesabu zilizokaguliwa ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha halmashauri hiyo kutakiwa kuandaa nyingine.
Kamati imeagiza halmashauri kurekebisha dosari zilizojitokeza, ikiwemo kukosekana nyaraka za mapato zenye thamani ya Sh2.3 milioni na kutokukusanya Sh208.7 milioni
kutoka kwa wakala bila ya hatua stahiki kuchukuliwa kwa mujibu wa
mkataba.

No comments:

Post a Comment