Wednesday, September 13

Wabunge kuondoa umri wa kuwania urais Uganda

Rasi Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionRasi Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.
Wabunge kutoka chama kinachotawala nchini Uganda NRM wamekubaliana kuwasilisha mswada ambao unapendekeza kuondewa miaka ya kuwania urais nchini Uganda.
Ikiwa watafaulu mswada huo utamwezesha Rais Yoweri Museveni ambaye anaaminika kuwa mwenye umri wa miaka 73, kuwania tena uchaguzi wa mwaka 2021.
Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa sasa anahudumu muhula wake wa tano madarakani.
Mswada ambao huo amabo unaungwa mkono na wabunge 200 wa NRM unataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha 102 (b) cha katiba ya Uganda, ambacho kinaweka umri ambao mtu anaweza kuwania urais wa kati ya miaka 35 na 75
Wengi wanasema kuwa NRM ambacho kina wabunge wengi, kitasababisha mabadiliko ya katiba lakini wengibe ndni ya NRM waekana.
Wabunge wanasema kuwa watawasilisha mswada huo bungeni katika kipindi cha wiki moja.

No comments:

Post a Comment