Virusi hatari vinavyoweza kusababisha madhara kwa ubongo wa watoto vinaweza kusaidia kwenye matibabu mapya kwa saratani ya ubongo kwa mtu mzima, kwa mujibu wa wanasayansi nchini Marekani.
Hadi sasa virusi vya Zika vinaonekana tu kuwa tisho la afya duniani.
Lakini utafiti wa hivi punde unaonyesha kuwa virusi hivi vinaweza kuvamia na kuua seli zinazosababisha saratani ya ubongo wa mtu mzima.
Majiribio yaliyofanyiwa panya yalionyesha kuwa virusi vya Zika vilikula seli za saratani ya ubongo.
Binadamu bado hawajafanyiwa utafiti huo, lakini wataalamu wanaamini kuwa virusi hiyo vinaweza kuingizwa kwa ubongo wa binadamu wakati wa upasuaji ili kuangamiza seli za saratani ya ubongo.
Pia matibabu hayo ya kutumia Zika yameonekana kufaulu kwenye sampuli za binadamu katika mahabara.
Kuna aina tofauti ya saratani ya ubongo. Aina ya Glioblastomas ndiyo maarufu zaidi kwa watu wazima na moja ya saratai ngumu zaidi kutibiwa.
Aina hii ya saratani husambaa kwa haraka, ikimaanisha kuwa ni vigumu kubaini imeanzia wapi na kuishia wapi.
Lakini utafiti wa hivi punde kwa panya walio hai na kwa sampuli za binadamu unaonyesha kuwa matibabu ya kutumia Zika yanaweza kuua seli ambazo ni sugu kwa matibabu ya kipindi hiki.
Wanasayansi wa Uingereza katika chuo cha Cambridge nao wameanzisha utafiti sawa na huo.
Dr Catherine Pickworth, kutoka taasisi ya utafiti wa saratani nchini uingereza anasema kuwa virusi vya Zika vilivyofanyiwa mabadiliko vinaweza kushambulia seli za saratani ya ubongo kwenye mahabara.
No comments:
Post a Comment