Wednesday, September 27

Twitter watangaza kuongeza maneno lakini watumiaji hawajafurahia


Mtandao wa Twitter umeatangaza kuwa upo katika majaribio ya kuongeza idadi ya herufi (character limit) kutoka 140 za sasa 280.
Meneja uzalishaji wa mtandao huo, Aliza Rosen amesema wanataka kuongeza idadi ya maneno ili watu waweze kujieleza kwa uhuru.
Katika hali isiyotarajiwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo hawajaipokea vizuri taarifa hiyo wakisema itaufanya ufanane na mingine.
Mwanzilishi wa Twitter, Jack Dorsey alikuwa wa kwanza kujaribu kuandika tweet yenye herufi 280 na kujibiwa na watuamiaji hao kuwa hiyo inapunguza ubunifu.
Din Moses wa Kenya alisema: “Herufi 240 zitapunguza ubunifu katika uandishi.” Mwingine anayejitambulisha kwa jina la Arsene Wenger aliandika: “Sitasoma tena tweet, sina muda wa kusoma maandiko marefu.”
Ciru Muriuki naye alimhoji Dorsey sababu za kuongeza maneno badala ya kuiwezesha Twitter kufanya marekebisho pale unapokosea katika andiko lako.
Katika mtandao wa Twitter unapokosea kuandika utalazimika kufuta kwa kuwa haiwezeshi kufanya marekebisho.
Mhariri wa Jarida la Vice la Marekani, Caitlin Kelly alikwenda mbali zaidi kuonyesha kuwa hakuridhika na uamuzi huo kwa kuipunguza maneno tweet ya Dorsey yakabaki 139 na kuleta maana ile ile.

Wengine walisema anayefurahia mabadiliko hayo ni Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kuwa hupenda kuutumia mtandao huo kuandika taarifa zake.

No comments:

Post a Comment