Tuesday, September 5

Ripoti madini ya Tanzanite, almasi kesho



Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai kesho atapokea ripoti ya kamati ya maalum mbili zilizoundwa kwa ajili ya kuchunguza biashara ya madini aina ya Tanzanite na almasi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kitengo cha Habari cha Bunge, Spika atapokea ripoti hizo na kisha kuzikabidhi kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kamati hizo ziliundwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge na Ndugai ambaye alizipa siku 30 kukamilisha kazi hiyo.
Pia wabunge watapokea taarifa ya Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo.
Taarifa hiyo inasema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Namba 3 wa mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Reli wa Mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka 2016.
Leo Bunge litaanza kwa kuwaapisha wabunge saba wa viti maalum wa CUF walioteuliwa hivi karibuni.
Wabunge hao ni Afredina Apolinary Kahigi, Kiaza Hussein Mayeye , Nuru Awadhi Bafadhali, Rukia Ahmed Kassim, Shamsa Aziz Mtamba, Sonia Jumaa Magogo, Zainab Mndolwa Amir.

No comments:

Post a Comment