Itakuwa vyema ikiwa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kitashindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2019, rais wa zamani Kgalema Motlanthe amesema.
"Chama hicho kimehusishwa na ufisadi na ni lazima kipoteze ili tatizo hilo kumazika," aliambia BBC.
Bwana Motlanthe ni mwanachama wa cheo cha juu wa ANC ambaye matamshi yake yanaonyesha kuwepo tofauti kubwa chamani.
Chama hicho kimeshinda kila uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 60 tangua utawala wa wachache ufikie kikomo mwaka 1994.
- Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela
- Rais wa zamani Afrika Kusini ampinga Jacob Zuma
- Rais Zuma aponea shinikizo za kumtaka ajiuzulu
Hata hivyo kilishindwa katika miii mikuu nchini Afrika Kusini ukiwemo mji wa Johannesburg wakati wa uchaguzi wa manispaa mwaka 2014.
Wapiga kura walionekana kukiadhibu ANC kutokana na ufisadi ufisadi unaozidi kukiandama.
Kiongozi wake Rais Jacob Zuma, ameponea kura ya kutokuwa na imani nae mara 8 katika bunge.
Amelaumiwa na upinzani na wakosoaji wengine wa ANC kwa kuwa kati kati ya mtandao wa ufisadi ndani ya serikali, madai ambayo anayakanusha.
No comments:
Post a Comment