Kim Jong-un amesema kauli za "wazimu'' rais wa Marekani Donald Trump zimemshawishi kuwa alikuwa sahihi kutengeneza silaha kwa ajili ya Korea kaskazini.
Katika kauli yake binafsi ambayo haikutarajiwa, kupitia vyombo vya habari vya taifa, Bwana Kim alisema kuwa Bwana Trump ''atalipia" hotuba yake ya hivi karibuni katika Umoja wa Mataifa.
Jumanne wiki hii rais wa Marekani alisema kwamba kama Marekani ikilazimishwa kujilinda ''itaiangamiza kabisa'' Korea Kaskazini.
Bwana Trump pia alimkejeli Bwana Kim akimuita "rocket man" anae andaa mpango wa ''kujiangamiza ".
Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya makombora, na ilifanya jaribio la sita la nuklia licha ya majaribio hayo kulaaniwa kimataifa.
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Ri Yong-ho, ambaye awali alilinganisha hotuba ya Bwana na "sauti ya mbwa anayebweka ", ameonya kuwa utawala wa Pyongyang unaweza kufanya jaribio la bomu la sumu ya nuklia aina ya katika bahari ya Pacific kujibu tisho la rais wa Marekani.
"Bomu hilo linaweza kuwa bomu zito zaidi la majini aina hiyo kuwahi kufyatuliwa katika bahari ya Pacific," Bwana Ri alinukuliwa na shirika la habari la Korea Kusini -Yonhap.
Hata hivyo aliongeza kusema kuwa:" Hatufahamu juu ya hatua gani zinaweza kuchukuliwa kama itakavyoagizwa na kiongozi Kim Jong-un."
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika malumbano makali katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment