Rais wa Zimabawe Robert Mugabe na mkewe Grace, wamekuwa watu wa kwanza kujiandikisha kama wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Rais hata hivyo alisema kuwa shughuli hiyo ya kujiandikisha ilichukua muda mrefu.
- Mugabe kuelekea Afrika Kusini kutatua kesi ya mke wake
- Grace Mugabe arudi Zimbabwe licha ya kutafutwa na polisi Afrika Kusini
Raia wote wa Zimbabwe wakiwemo wale waliopiga kura kwenye uchaguzi uliopita, watahitaji kujiandikisha upya kwa kutumia mfumo mpya ambao unachukua alama za vidole na picha za uso.
Ni vifaa 400 kati ya 3000 vya kuwandikisha wapiga kura vilivyowasilishwa nchini humo kutoka China kwa shughuli hiyo ambayo itakamilka mwezi Januari mwaka 2018.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa inalenga kuwaandikisha watu milioni 7.
Bwana Mugabe ambaye ameingoza nchi tangu mwaka 1980, anatarajiwa kuwa mgombea wa chama cha Zanu-PF kwenye uchaguzi huo ambao unatarajiwa kuandaliwa kati kati mwa mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment