Raia wa uholanzi, Monique Honsbeek Amanzi, ameieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, rafiki yake wa kiume ambaye ni askari polisi kitengo cha Trafiki amemchania hati yake ya kusafiria.
Amanzi (28), amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa alifikishwa mahakamani hapo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuishi nchini bila ya kuwa na kibali.
Akisomewa mashtaka yake na wakili wa serikali kutoka ofisi za Uhamiaji, Nivatus Mlay amedai, Septemba 11 mwaka huu (2017) katika makao makuu ya ofisi za uhamiaji mshtakiwa huyo, akiwa raia wa Uholanzi alikutwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali. Baada ya kumaliza kusomewa tuhuma zake hizo.
Aliulizwa kama ni kweli au la, ndipo Amanzi akadai kuwa, alikuwa na hati yake ya kusafiria ambayo rafiki yake huyo wa kiume trafki aliyemtaja kwa jina la Letiko Kulwa wa Makumbusho Victoria aliichana na hivyo kumfanya asijue kama visa yake ilikuwa imeisha.
Amedai, alikuja nchini akitokea uholanzi akiwa na mumewe Ibrahim Abasa, na watoto wao wawili lakini baadae waliachana ndipo akampata trafiki huyo ambaye walizaa nae mtoto mmoja lakini alifariki.
Amedai ameishatoa taarifa katika kituo cha polisi miaka miwili iliyopita juu ya kuchanwa kwa hati yake lakini RB aliyopewa ameipoteza. Pia alishaenda kutoa taarifa Uhamiaji lakini hakupata msaada wowote.
Kesi hiyo itatajwa Septemba 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment