Ni ndoto iliozaa matunda kwa pacha walioshikana Maria na Consalata nchini Tanzania baada ya kuanza masomo yao katika chuo kikuu ili kujifunza kuwa walimu.
Kulingana na gazeti la The Citizen, waliwashukuru walimu wao wapya kwa mapokezi mema waliopata mbali na mazingira mazuri ya kusoma waliopata yalioandaliwa na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University.
Waliwasili katika chuo hicho mbele ya wanafunzi wengine ili kuweza kujiandaa na mazingira yaliyopo.
Walianza masomo yao ya Kompyuta siku ya Jumatano .Waliwashukuru Wamishenari wa Consalata kwamba wamefikia kiwango hicho cha maisha yao.
Wamishenari hao waliwalea na kuwashawishi kuendelea na masomo.
Mtawa mmoja katika Chuo hicho amesema kuwa kuwasili kwa pacha hao mbele ya wanafunzi wengine katika chuo hicho kutawawezesha kujiandaa ili kuweza kuwa sawa na wengine.
Vyumba vitatu vilivyopo na fanicha zote vimeandaliwa kwa pacha hao, ikiwemo jiko na sebule.
Naibu Chansela anayesimamia maswala ya fedha na usimamizi wa chuo hicho , Fr Kelvin Haule alionyesha furaha baada ya kuwapokea pacha hao.
Amesema kuwa masomo yataanza mwisho wa mwezi Oktoba lakini masomo ya kompyuta yanaanza mara moja.
No comments:
Post a Comment