Thursday, September 28

Mwanamke ajioa



Picha kwa hisani ya mtandao wa BBC

Picha kwa hisani ya mtandao wa BBC 
Mwanamke raia wa Italia, Laura Mesi (40) amejioa na kufanya sherehe yenye waalikuwa 70
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, mwanamke huyo amesema ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaamini kuwa lazima mtu ujipende kwanza.
Laura amesema wazo la kufunga ndoa mwenyewe lilimjia miaka miwili iliyopita baada ya uhusiano wake wa miaka 12 kuisha.
“Niliwaambia marafiki na familia kama sitapata mchumba nikifikia miaka 40 basi nitajioa,” ameliambia gazeti la La Repubblica.
“Kama siku moja nitapata mwanaume ambaye nitakuwa na mipango naye, nitafurahi, lakini furaha yangu haitamtegemea yeye.”
Laura amesema yeye ndiye mwanamke wa kwanza Muitaliano kujioa mwenyewe. (BBC)

No comments:

Post a Comment