Wednesday, September 20

MWAKILISHI KUTOKA BENKI YA DUNIA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MABORESHO WA HUDUMA ZA KIMAHAKAMA

Na Mary Gwera, Mahakama

Mwakilishi ‘Practice Manager’ kutoka Benki ya Dunia (WB), Bw. George Larbi ameisifu Mahakama kwa utekelezaji wake wa Mradi wa Maboresho wa huduma za Kimahakama.

Bw. Larbi aliyasema hayo mapema Septemba 19, alipokutana na Mhe. Jaji Mkuu ofisini kwake Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam ambapo alipata nafasi ya kuongea na Mhe. Jaji Mkuu na Viongozi wengine wa Mahakama akiwemo Mtendaji Mkuu na Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

“Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama ni mradi wa mfano ambapo mafanikio yake yanatarajiwa kuigwa nan chi nyingine,” alisema Bw. Larli.

Bw. Larli ambaye amewasili nchini kutokea Washington D.C zilipo ofisi cha Benki ya Dunia amefanya ziara yake kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).

Alisema Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama ni Mradi wa pili kwa nchi za Afrika ambapo Benki ya Dunia inashirikiana moja kwa moja na Mahakama katika kuboresha huduma ya utoaji haki.

Maeneo muhimu yanaotekelezwa na Mradi wa Benki ya Dunia (WB) ni pamoja na; Mapambano dhidi ya Rushwa; ni kwa jinsi gani Mahakama pamoja na wadau wengine wanaweza kushirikiana katika kupiga vita vitendo vya rushwa.Maeneo mengine ni ushirikishaji wa wadau katika masuala yote ya utoaji haki na kusogeza huduma ya utoaji haki karibu na wananchi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibarhim Hamis Juma (kulia) akiongea neno na Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia (katikati) wa kwanza kushoto ni Bw. Denis Biseko 'Co-Team Task Leadear' wa Mradi wa Maboresho ya Huduma za Kimahakama.
 Bw. George Larbi, kutoka Benki ya Dunia (WB) (katikati) akiongea na Mhe. Jaji Mkuu (kulia).
 Mhe. Jaji Mkuu (aliyeketi wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wageni kutoka Benki ya Dunia (wawili walioketi katikati) wa tatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hussein Kattanga, wa pili kushoto ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mradi wa Maboresho wa Huduma za Mahakama, Mhe. Zahra Maruma.
 Ukaguzi: Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mahakama cha Mahakama-Kisutu unaojengwa kwa fedha za Benki ya Dunia Bw. George Larbi kutoka Benki ya Dunia pia alipata fursa ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Mahakama unaofanyika katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa sasa kazi ya upakaji rangi katika jengo hilo inaendelea.
 Mafundi wakiendelea na kazi ya upakaji rangi katika jengo la Kituo cha Mafunzo linalojengwa Kisutu-Dar es Salaam (Picha na Mary Gwera, Mahakama) 

No comments:

Post a Comment