Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi leo na kumuona Masogange ana kesi ya kujibu hivyo anapaswa kujitetea.
Uamuzi huo ameutoa baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.
Baada ya uamuzi wa Mahakama, Masogange alieleza atajitetea kwa njia ya kiapo na anatarajia kuwaita mashahidi watatu. Anatetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Ruben Simwanza.
Upande wa mashtaka unaowakilishwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula uliwaita mashahidi watatu.
Masogange (28) anayekabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin naOxazepam ataanza kujitetea Oktoba 12.
No comments:
Post a Comment