Marekani imesema kwamba inahitaji takriban dola milioni mia saba zaidi kuweza kutoa misaada ya kibinaadam nchini Syria.
Wizara ya habari imesema zaidi ya dola milioni mia tano itasambazwa kote Syria.
Fedha nyingine zitapelekwa nchi jirani zinazosaidia kuhifadhi wakimbizi wa Syria zikiwemo Lebanon, Jordan na Uturuki zinazohifadhi zaidi ya raia milioni tano wa Syria.
Hii inafikisha idadi ya dola bilioni saba tokea Marekani ilivyoanza kutoa misaada yake mwaka 2011 kwa Syria.
No comments:
Post a Comment