Sunday, September 3

Majaliwa kuzindua mfumo wa uandaaji bajeti


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Jumanne Septemba 5 atazindua mifumo miwili itakayosaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama wakati wa ufuatiliaji na uandaaji wa bajeti nchini.
Katika uzinduzi huo, mawaziri sita ambao wanafanya kazi na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) watahudhuria.
Kiongozi wa timu ya rasilimali fedha, Dk Gemini Mtei amesema uzinduzi huo utahudhuriwa na Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene; Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango; Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, bunge, kazi, vijana, na watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama.
Ofisa Usimamizi Mwandamizi wa Fedha Tamisemi, Elisa Rwamingo amesema mfumo huo utatumika katika halmashauri zote 185. Amesema wakuu wa vitengo katika halmashauri wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa mfumo huo, ambao wataenda kuwafundisha watumishi wengine.

No comments:

Post a Comment