Thursday, September 21

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAMUACHIA HURU MBUNGE WA BUKOBA MJINI, WILFED LWAKATARE

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfed Lwakatare baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Kuwasilisha hati ya kuondoa shauli hilo kwa kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yake.

Lwakatare ambaye kesi yake imedumu kwa zaidi miaka minne alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kula njama kutenda kosa

Akiwasilisha hati hiyo mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba, wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameeleza kuwa wanaomba kesi hiyo iondolewe chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kilichofanyiwa marekebisho 2002 sababu (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema ameifuta kesi hiyo na mshtakiwa(Lwakatare) yupo huru.Mapema, DPP aliondoa maombi yake dhidi ya Lwakatare, kuhusiana na shtaka la ugaidi katika Mahakama ya Rufaa.

Katika maombi hayo DPP aliomba kibali cha kufungua mapitio kuhusiana na uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi.

Katika kesi hiyo, Lwakatare na mwenzake Ludovick Rwezaura, walikuwa wakikabiliwa na jumla ya mashtaka manne likiwemo la kula njama za kufanya vitendo vya kigaidi kwa lengo la kumdhuru kwa sumu aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.

No comments:

Post a Comment