Dar es Salaam. Kampeni ya siku tano ya upimaji wa afya bure imeanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini hapa.
Upimaji huo utakaohitimishwa Septemba 10 unaendeshwa na madaktari bingwa na wauguzi zaidi ya 200 kutoka hospitali za umma, Jeshi na za watu binafsi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema jana Septemba 5 kuwa upimaji wa afya bure unalenga kuwapatia wananchi fursa ya kujua hali zao na kuwa na utaratibu wa kupima mara kwa mara.
Amesema kutakuwepo vifaa tiba vya kisasa, magari ya kubeba wagonjwa, vyoo, sehemu za watoa huduma na za kupumzika wakati wa kusubiri huduma.
No comments:
Post a Comment