Friday, September 15

Chanjo ya watoto huenda ikatolewa mara moja

Chanjo ya watoto huenda ikatolewa mara moja
Image captionChanjo ya watoto huenda ikatolewa mara moja
Teknolojia ambayo huenda ikapelekea chanjo ya watoto kutolewa mara moja kwa kila mtoto imebuniwa na watafiti nchini Marekani.
Chanjo hiyo itakayotolewa mara moja kwa mpigo itashirikisha dawa zote katika sindano moja ambazo zitakuwa zikifanya kazi kwa muda utakaohitajika ili kumkinga mtoto na magonjwa yanayolengwa.
Teknolojia hiyo imeonakana kufanya kazi miongoni mwa panya katika jarida la sayansi.
Watafiti wanasema teknolojia hiyo inaweza kuwasaidia wagonjwa duniani.
Chanjo ya watoto husababiha vilio na machozi na nyingi hupewa watoto kwa muda tofauti.
Kundi moja la watafiti katika chuo cha kiteknolojia cha Massachusetts kimebuni chanjo ambayo inashirikisha dawa zote za chanjo anayopewa mtoto.
Dawa hiyo imetengezwa katika hali ambapo chanjo zilizochanganywa hujitokeza na kuanza kufanya kazi katika muda tofauti katika kiupindi cha wiki sita licha ya kutolewa kwa pamoja.
Teknolojia hiyo itawasaidia wazazi ambao hawana uwezo wa kwenda hospitalini mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment