Wananchi zaidi ya 1,000 wameathirika na bomoabomoa hiyo iliyoanza leo Ijumaa saa tatu asubuhi.
Akizungua katika eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema serikali ya wilaya imetimiza agizo la kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa cha Oktoba mwaka jana kilichotangaza wananchi hao wahamishwe katika maeneo hayo.
Wakizungumza na waandishi baadhi ya wananchi balozi wa eneo hilo Cleofas Vitalis amesema wanaishi katika eneo hilo toka mwaka 2002 na walinunua maeneo kutoka kwenye uongozi wa Mtaa wa Mkoani ambao zamani kilikua Kitongoji cha Mkoani.
Amesema wamepewa taarifa ya kutakiwa kuhama maeneo hayo miezi miwili iliyopita lakini hawakuhama wakiamini Serikali itawahurumia kwa kuwa hawana pa kwenda na tayari wana watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Mkoani.
Wanafunzi zaidi ya 100 wanaosoma Shule ya Msingi Mkoani wameathiriwa na bomoabomoa hiyo.
No comments:
Post a Comment