Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali imesema kuwa Baraza la Taifa la Ujenzi ni muhimu kwa taifa pamoja na kwa wananchi katika kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ujenzi nchini.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakati akifungua warsha ya Baraza la Taifa la Ujenzi kujadiliana la maboresho ya baraza hilo, uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa hakuna mtu ambaye anajua gharama ya mraba wa mita moja ambapo kazi hiyo ilitakiwa kufanywa na baraza hilo.
Amesema kuwa wakati mtu anataka kujenga nyumba anaweza kupata gharama katika baraza la ujenzi na kuachana na ujenzi wa mazoea ambao unachukua gharama kubwa.
Mbarawa amesema bidhaa zinaingia nchini lakini hakuna anayejua gharama na ubora na kutofautisha na bidhaa zingine za ambapo kazi hiyo baraza la taifa la ujenzi linatakiwa kufanya.
Amesema kuwa kama mambo hayaendi sawa kutokana na sheria yuko tayari kubadilisha sheria ili baraza lifanye kazi yake kwa maendeleo ya taifa.
Aidha Mbarawa amesema warsha hiyo italeta mapendekezo ya kina kutokana na wadau waliopo katika sekta ya ujenzi ili iweze kuleta matokeo chanya.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema warsha hiyo watajadili katika kuborseha baraza hilo.
Amesema kuwa wadau wa sekta ya ujezi watakuwa huru na wazi katika uchangiaji masuala mbalimbali ikiwa na malengo ya kuborsesha sekta ya ujenzi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Mayunga Mkunya amesema kuwa kufanyika kwa baraza hilo ni matokeo kile kitachojadiliwa kuwezesha katika kujenga baraza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kujadili mabaoresho ya baraza la taifa la Ujenzi lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza juu ya baraza la Taifa la Ujenzi linavyofanya kazi leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Profesa Mayunga Mkunya akizungumza juu warsha hiyo itavyoleta matokeo yaliyotokana na majadiliano na wadau leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau ya wakiwa kwenye Warsha ya Baraza la Taifa la Ujenzi kujadiliana maboresho ya baraza hilo, iliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa warsha ya baraza la Taifa la Ujenzi leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment