Kesi hiyo imetajwa leo Jumanne mbele ya Jaji Modester Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ambapo Nangole amewakilishwa na wakili John Mallya kwa niaba ya Tundu Lissu na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Stivin Kiluswa aliwakilishwa na wakili Daud Haraka.
Jaji Opiyo baada ya kueleza kupokea maombi ya warufani namba 108/2017 aliwataka mawakili wa pande zote kujibu kutoa hoja zao kwa maandishi.
Mawakili upande wa rufaa wametakiwa kuwasilisha hoja zao Oktoba 3 na upande wa utetezi wanapaswa kujibu kwa maandishi hoja zao Oktoba 10 mwaka huu.
Jaji Opiyo amesema Oktoba 16 pande zote watafanya majumuisho ya hoja na Oktoba 17 itapangwa tarehe ya kusikilizwa maamuzi.
No comments:
Post a Comment