Uzinduzi huo umefanyika leo Jumanne Agosti Mosi makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam na umekwenda sanjari na kuhamasisha Watanzania kufahamu kwa undani majanga ya moto na namna ya kukabiliana nayo
Kamishana Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye, amewaambia wanahabari kuwa namba hizo zitawasaidia Watanzania kupiga simu na kupatiwa huduma za uokozi haraka.
"Watu wengi wanaifahamu namba 112 ambayo ni polisi lakini 114 hawaifahamu vizuri, hali inayosababisha kutumia muda mwingi kupiga 112 badala ya 114. Nina imani sasa hivi watakuwa wanaitumia namba hii," anasema Kamishna Andengenye.
Amesema uzinduzi huo wa kampeni unakwenda sambamba na mchakato wa kuwajengea uewela Watanzania wa namna ya hatua za kuchukua na kukabiliana na majanga ya moto
Katibu Mtendaji wa United Against Crime, Andrew Elliot amesema wameamua kuweka nguvu katika kampeni ili kuokoa Watanzania na majanga ya moto na kwamba kupitia mchakato huo Watanzania watajengewa uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga hayo.
Elliot amesema katika kampeni hiyo wamesharikiana na watu mbalimbali ikiwamo kampuni ya Mabati ya Alfa na Selc
No comments:
Post a Comment