Friday, August 18

WAZIRI UMMY MWALIMU AENDELEA NA ZIARA MKOANI KATAVI



Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ameendelea na ziara yake mkoani Katavi, akiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kukagua huduma za Afya zitolewazo nchini.

Katika ziara hiyo Waziri huyo ametembelea kituo cha Afya Nsimbo na Inyonga katika Halmashauri ya Mlele na Usevya Halmashauri ya Mpimbwe. 

Akiwa katika vituo hivyo Waziri huyo alifanya ukaguzi kwenye maendeo mbalimbali ya utoaji huduma,upatikanaji was Dawa na vifaa Tina,miundombinu ya vituo hivyo pamoja na kuongea na watumishi wa Afya kujua changamoto zinazowakabili na kufanyia ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Aidha,akizungumza na watumishi hao,Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha kuwa dawa zinawafikia wananchi katika vituo vyote vya kutolea huduma.

Waziri huyo amekua akisisitiza Mara kwa Mara katika ziara zake suala ya usimamizi wa Dawa na vifaa Tiba kwenye hospitali na vituo vya Afya nchini ili kuondoa malalamiko mengi toka wa wananchi wanaofika kupatiwa huduma.

Kesho Waziri ataendelea na ziara take Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa

No comments:

Post a Comment