Washukiwa wa ugaidi ambao waliendesha mashambulilizi nchini Uhispania walikuwa wamekusanya mitungi 120 na walikuwa wakipanga kuitumia kwenye mashambulizi ya magari, kwa mujibu wa polisi nchini Uhispania.
Mitungi hiyo ilipatikana ndani ya nyumba ambayo inadaiwa kutumiwa na magaidi hao katika mji wa Alcanar siku ya Jumatano usiku.
Polisi bado wanamtafuta dereva wa gari ambalo liligonga watu kadha katika eneo la Las Ramblas mjini Barcelona na kuwaua 13.
Leo Jumapili misa ilifanyika mjini Barcelona kuwaomboleza waathiriwa.
Kando na watu 13 waliouawa siku ya Alhamisi huko Las Ramblas, mwanamke mwingine aliuawa wakati wa shambulizi la pili la gari mapema Ijumaa katika mji wa Cambrils.
Washukiwa watano magaidi waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye shambuliza hilo la pili.
Polisi wamethibitisha kuwa bado wanamsaka Younes Abouyaaqoub, mzaliwa wa Morocco, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.
No comments:
Post a Comment