WALLACE KARIA ASHINDA URAIS WA TFF, MICHAEL WAMBURA KUWA MAKAMU WAKE
Azam TV – Hotuba ya kwanza ya Rais mpya TFF Wallace Karia mjini Dodoma
Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF umehitimishwa kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia (kulia) kushinda kwa jumla ya kura 95 na kuwabwaga wapinzani wake.
Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani Dodoma ukiwa wa amani kwa wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na wagombea wenyewe.
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli akitangaza matokeo hayo ambapo alimtangaza Wallace Karia kama mshindi wa kinyang'anyiro kwa kura 95 kati ya kura 127 zilizopigwa.
Kuuli ametangaza kuwa, katika nafasi ya makamu wa Rais, Michael Richard Wambura (kushoto) ameshinda nafasi hiyo kwa kura 85.
Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu kumekuwa na maingizo mapya kutoka kanda mbalimbali za nchini kama ifuatavyo:
Zone 1: Saloum Chama
Zone 2: Vedastus Lufano
Zone 3: Mbasha Matutu
Zone 4: Sarah Chao
Zone 5: Issa Bukuku
Zone 6: Kenneth Pesambili
Zone 7: Elias Mwanjala
Zone 8: James Mhagama
Zone 9: Dunstan Mkundi
Zone 10: Mohamed Aden
Zone 11: Francis Ndulane
Zone 12: Khalid Abdallah
Zone 13: Lameck Nyambaya
No comments:
Post a Comment