Wakizungumza jijini hapa leo Agosti 31, baadhi ya wananchi waliowawakilisha wenzao wamesema hali imekuwa mbaya baada ya makazi yao kuanza kuchomwa moto.
Mwakilishi wa wenyeviti wa mitaa, Lazaro Malongo amesema licha ya eneo lao kuwa kwenye mgogoro kwa zaidi ya miaka 20, Serikali inapaswa kusitisha uchomaji wa makazi ili kunusuru maisha ya wananchi wasio na pa kwenda.
Mwakilishi wa wanawake wa eneo hilo, Pirias Maingo amesema hali si shwari kwao na watoto kutokana na kukosa makazi baada ya nyumba kuchomwa.
"Twende wapi sasa, tumekuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu wenyewe. Tunaomba Waziri Mkuu atusaidie," amesema.
No comments:
Post a Comment