Saturday, August 12

UCHAGUZI MKUU TFF- MAGUFULI NDIYE ATAKAYE TULETEA RAIS WA KUKUMBUKWA TFF



.
Na Honorius Mpangala.

Ni katika utawala wa Rais wa awamu ya tano Dodoma imerejesha Hadhi yake kama makao makuu ya nchi tangu ilivyokuwa hivyo kwa zama za Mwalimu J. K. Nyerere. Hadhi ya Dodoma inamfanya kila mmoja atamani kuishi Dodoma.

Ni katika utawala wa awamu ya tano ambapo uchaguzi wa TFF unawaingiza viongozi wapya madarakani. Hakuna asiyeijua kasi ya kiutendaji pamoja na heshima ya ofisi za umma zilivyo kwa sasa.

Viongozi watakao chaguliwa moja kwa moja wataingia madarakani kwa kutambua kiongozi mkuu wa nchi ni nani. Hakuna kiongozi ambaye atakuja kufanya tofauti katika utawala huu kama ikitazamwa viongozi watangulizi hadi niandikapo wako rumande.

Wanataka kutufikisha sehemu fulani wanatuhaidi mabadiliko lakini kitu pekee ambacho tutapaswa kujiandaa nacho ni pale tutakapo ambiwa mambo yanayohusu fedha lazima yakaguliwe na CAG.Hili ni jambo la kujipanga nalo na kwa viongozi watakao ingia madarakani naamini lazima akili yao itakuwa imesoma alama za nyakati na kutambua mahitaji yaliyopo sasa.

Ikiwa kama shirikisho linahitaji mchango wa serikali katika kufanikisha Yale matarajio basi wasisite kutoa ushirikiano pia itakapofika wakati wa kuhitaji ukaguzi wa kiofisi.Miongoni mwa mambo yanayoendelea katika shirikisho letu ni upatikanaji watu mwenye weredi katika kusukuma maendeleo ya soka letu.

Wakati Rais mstaafu Bemjamini William Mkapa anatoweka madarakani mwaka 2005 alicha Uwanja wa taifa. Wakati Rais mstaafu pia Jakaya Kikwete anatoweka madarakani mwaka 2015 aliacha utaratibu wa Kocha mkuu wa timu ya taifa akilipwa mshahara na serikali. 

Awamu ya nne licha kufanikisha kwa kuzisaidia timu zetu za taifa kwa kuwaleta walimu toka nje ya Tanzania lakini tulikosa watu wa kuwachunguza watu tuliowapa mamlaka ya kusimamia vyama hivyo vya Michezo.

Alikuja kocha wa ngumi toka nchi ya Cuba hadi Leo hakuna mwenye majibu yaliyonyooka aliondoka vipi. Sio kocha wa ngumi tu bali hata kocha wa Netball alikuja hapa nchini lakini Uswahili wa viongozi wetu hakuna ambaye alielewa.

Awamu hii Rais kafanikiwa kumshawishi mfalme wa Morocco kuweza kufanikisha upatikanaji wa uwanja wa Michezo pale Dodoma. Ni kitu kikubwa sana kufanyika ambacho kitaifanya Dodoma kujikuta ikimpa heshima ya juu Rais wetu kwa maamuzi yake na Uzalendo wake kwa taifa lake.

Katika kipindi hiki ndipo niligundua Waziri wa wizara ya Michezo anawasiliana na watu wa FIFA na kuwaeleza kila wafanyalo kwa shirikisho la Mpira la Tanzania ni lazima serikali ifahamishwe. Hali hii itapelekea kufanikisha mambo mengi yaliyokuwa yanaelekeza katika utekelezaji wa miradi ya TFF.



Kwa viongozi watakao ingia madarakani watakuwa na uwepesi wa kazi kutokana na kuzisoma nyakati na kujua mahitaji na kiu ya watanzania katika msuala ya Michezo. Nina hakika kwa kiongozi yeyote atakaye fanikiwa kuingia katika uongozi atakuwa amesoma nyakati vyema.Utendaji wa shirikisho utakuwa na ufanisi sana.

Soka letu linahitaji MTU amayeweza kujitoa kwaajili ya watu ili kufanikisha ndoto zao. Tunahitaji MTU anatakaye tambua uwezo na kipaji cha vijana walioko kwenye mfumo wa kimakuzi katika soka. Hadi sasa ilikuwa inashangaza vijana waliokuwa wamepelekwa katika vituo vya kulelewa kisoka kutotumika. Wako waliopelekwa Nchi ni Ghana na mwingine pale Dakar Senegal lakini hakuna anayeonekana kuwakumbuka vijana wale.

Ni kama tunapiga konzi kwenye kinyago na hatimaye tunaumia wenyewe. Tunahitaji atakaye tujuza kuwa hiki ni kinyago na tuachane nacho kukipiga makonzi. Shirikisho lenye uthubutu katika utendaji ndio mafanikio ya soka letu.Natamani kuona serikali ikiwa na mamlaka ya kushirikiana na TFF katika kufanikisha kila jambo. Kwa taasisi iliyo chini ya serikali ingekuwa safi kuona mkaguzi wa hesabu za serikali akifanya kazi katika nyanja mbalimbali katika masuala ya Michezo.

Hoja ya kusambaza mpira nchi nzima itaweza kusaidia hata kufanya hata baadhi ya maeneo yanayo onekana hayana soka basi watacheza soka. Kuto kuwa na soka ni hali ya mikoa kutokuwa vilabu kwa daraja la kwanza la pili hata ligi kuu.

Rais wa TFF unayekuja pamoja na wajumbe wako jambo pekee la kuweka kichwani ni kwamba Rais Wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli anakusubili mfanye kazi mfanikishe ujenzi wa Uwanja wa Michezo pale Dodoma.


No comments:

Post a Comment