Thursday, August 24

Trump: Korea Kaskazini imeanza kutuheshimu

Rais Donald Trump amesema kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo kati ya Marekani na Korea Kaskazini
Image captionRais Donald Trump amesema kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo kati ya Marekani na Korea Kaskazini
Rais Donald Trump amesema kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo katimya Marekani na Korea kaskazini.
Akimtaja rais Kim Jong un , Trump amesema kuwa : Ninaheshimu ukweli kwamba ameanza kutuheshimu.
Aliongezea: Pengine sio ukweli, lakini kuna matumaini
Hivi majuzi rais Trump aliitahadharisha Korea Kaskazini kwamba inafaa kuwa na "wasiwasi sana" iwapo itatenda lolote kwa Marekani.
Alisema utawala wa taifa hilo utakuwa shida kubwa "ambayo ni mataifa machache sana yaliyowahi kukumbana nayo" iwapo "hawatabadilika".
Rais Donald Trump amesema kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo kati ya Marekani na Korea Kaskazini
Image captionRais Donald Trump amesema kuna matumaini kuhusu kupungua kwa wasiwasi uliokuwepo kati ya Marekani na Korea Kaskazini
Trump alisema hayo saa chache baada ya Korea Kaskazini kutangaza kwamba ina mpango wa kurusha makombora manne karibu na kisiwa cha Marekani cha Guam.
Korea Kaskazini imesema mpango wake wa kufyatua makombora kwenda kisiwa cha Marekani cha Guam, utakuwa tayari hivi karibuni huku majibizano ya kivita kati yake na Marekani yakiendelea.
Vyombo vya habari vilisema kuwa makombora ya Hwasong-12 yatapita anga ya Japan na kuanguka baharini karibu kilomita 30 kutoka kisiwa cha Guam ikiwa mpango huo utaidhinishwa na Kim Jong-un.

No comments:

Post a Comment