Saturday, August 12

Trump amshukuru Vladimir Putin kwa kuwafukuza wanabalozi

Ubalozi wa Moscow, Russia, on 28 Julai 2017

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionUrusi imesema maafisa wa kibalo wa Marekani watatakiwa kuondoka kufikia tarehe 1 Septemba
Rais wa Marekani Donald Trump amemshukuru Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuagiza kuondoka kwa wafanyakazi 755 kutoka kwenye afisi za kibalozi za taifa hilo nchini Urusi.
Akiongea na wanahabari New Jersey, kiongozi huyo amesema angependa kumshukuru sana kiongozi huyo wa Marekani kwa kuisaidia Marekani kuokoa fedha.
Uchunguzi unafanyika nchini Marekani kubaini iwapo kulikuwa na ushirikiano kati ya maafisa wa kampeni wa Trump na Urusi, inayodaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Bw Trump ameshutumu uchunguzi huo.
Mwishoni mwa mwezi Julai, Rais Putin alisema wafanyakazi 755 wangelazimishwa kuondoka kutoka afisi za kibalozi za Marekani nchini Urusi, akilipiza kisasi hatua ya Marekani kuiwekea Moscow vikwazo zaidi.
Wengi wa wafanyakazi hao ni waajiria wa kutoka Urusi, ikiwa na maana kwamba watu ambao watalazimishwa kuondoka nchini humo hawafiki 755.
Alisema watatakiwa kuondoka kufikia tarehe 1 Septemba, na kufikisha idadi ya wafanyakazi katika afisi za kibalozi wa Marekani hadi 455, sawa na wafanyakazi wa kibalozi wa Urusi walio Washington.
Russian President Vladimir Putin and his US counterpart Donald Trump at the G20 summit in Hamburg, 7 July 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPutin na Trump walikutana mjini Hamburg Ujerumani Julai

Shukrani

Wafanyakazi katika ubalozi wa Marekani mjini Moscow, pamoja na afisi za kibalozi katika miji ya Ekaterinburg, Vladivostok na St Petersburg wameathiriwa.
Wakati huo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitaja hatua hiyo kuwa ya kusikitisha na isiyofaa.
Lakini Bw Trump amemshukuru Bw Putin kwa kupunguza wafanyakazi wanaolipwa mishahara na serikali ya Marekani.
"Ningependa kumshukuru kwa sababu tunajaribu kupunguza wafanyakazi wetu na kwangu mimi namshukuru sana kwamba amewafukuza watu wengi kiasi hicho," amesema.
Aidha, Alhamisi, Rais Trump alisema alishangazwa sana na uvamizi uliofanywa katika nyuma ya mwenyekiti wake wa zamani wa kampeni Paul Manafort jimbo la Virginia na maafisa wa uchunguzi wa Marekani.
Mwanasheria maalum Robert Mueller, anayeongoza uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba Marekani iliingilia uchaguzi wa Urusi, aliondoka nyumani kwa Manafort mjini Alexandria akiwa na "nyaraka kadha" kwa mujibu wa gazeti la Washington Post.

No comments:

Post a Comment