Mradi huo unafadhiliwa na Jiji la Hamburg nchini Ujerumani na utagharimu zaidi ya Sh4 bilioni.
Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta amesema hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi atakayejenga kiwanda hicho eneo la Mabwepande.
Amesema ujenzi utafanyika kwa miezi 12 na ukikamilika utatoa ajira kwa vijana mkoani Dar es Salaam.
"Katika mradi huu manispaa tunatakiwa tutenge eneo la ujenzi na kugharimia miundombinu ya barabara, maji na umeme na ndicho tutakachokifanya," amesema.
Sitta ambaye pia ni diwani wa Msasani (CCM), amesema mradi ukikamilika utasaidia pia kupunguza taka kwenye masoko ya manispaa hiyo.
Amesema mradi utaongeza mapato ya manispaa kutokana na mbolea itakayozalishwa.
No comments:
Post a Comment