Friday, August 25

Soko la Wazi la Mkulima Market Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanza Agosti 30 hadi septemba 2, 2017


25 Agosti 2017
Ni msimu mwingine wa Soko la Wazi la Mkulima Market maarufu kama Mkulima Soko. Tunakukaribisha kuungana na wazalishaji na wachakataji bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji kuona wazalishaji kutoka kila pembe ya Tanzania. Katika Mkulima Soko utapata fursa ya kuona, kupata elimu na kununua bidhaa bora zinazozalishwa Tanzania.

Soko hili la Wazi litafanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi 2 Septemba 2017 (Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi). Karibu ujifunze ufugaji wa sungura, samaki na nyuki. Kama kawaida soko litafanyika kwenye Maegesho ya Magari ya Research Flats, mbele ya Jengo la Ndaki ya Kilimo na Teknolojia za Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Msimu huu kutakuwa na wazalishaji wapatao 60 watakaoleta bidhaa mbalimbali fresh na zilizochalatwa.

Katika soko hili kutakuwa na mambo makubwa manne:

1.     Mkulima Market itazindua rasmi kidokozi (app) pamoja tovuti yake ya mkulimamarket.com ili kuwezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo, Uvuvi, Ufuaji na Uwindaji.
2.     Uzinduzi wa masoko ya wazi ya kila mwisho wa wiki yatakayofanyika kwenye eneo la Organic Farmer Supermarket iliyopo eneo la Kijitonyama mita 300 toka kwenye taa za Sayansi, mkabala na Hoteli ya Colubus. Hivyo basi wakati wa soko la wazi, wazalishaji watapata fursa ya kujiunga na mtandao huu mkubwa wa wazalishaji wa bidhaa zenye ubora kutoka shambani hususani nyanya, vitunguu, pilipili hoho, karoti, viazi, mchele, unga wa mahindi, kuku samaki na asali.
3.     Uhabarishaji kuhusu huduma mpya ya kupata bidhaa mlangoni kwako iitwayo Mkulima Basket kwa kushirikiana na Organic Farmer Supermarket.
4.     Pia tutakuwa elimu kuhusu ufugaji sungura itakayotolewa Uhuru Rabbits.  Pamoja na kutoa elimu kuhusu ufugaji wa sungura wataendesha onesho la kuonja nyama choma ya sungura.

Tunamkaribisha kila mwana Dar es Salaam kuja kuona ubunifu na maendeleo yanayotokana na biashara katika sekta kilimo nchini Tanzania. Kama kawaida kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na michezo ya watoto. Hakuna kiingilio

Unaweza kuwasiliana na Mratibu kupitia namba 0767 254 887 au 0629 042 678 au kwa kuandika barua pepe kupitia mkulimamarket@gmail.com au kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, facebook, instagram na youtube.

Shukrani za kipekee kabisa ziende kwa Kilimanjaro Audiovisual Services (KAVS), Michuzi Blog, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na TanTrade kwa kuendelea kuuunga mkono kazi za Mkulima Market.

No comments:

Post a Comment