Monday, August 7

Selcom yaipa shavu T-Junction ya Kijiweni Production

Uzinduzi wa filamu hiyo ambayo wahusika wake nji wasanii wa hapa nchini, umewezekana kutokana na ufadhili kutoka kampuni kadhaa ikiwemo Selcom.

Kampauni ya uzalishaji wa filamu ya Kijiweni Productions wiki hii itazindua filamu yake mpya ya T-Junction katika ukumbi wa Molimani City.
Uzinduzi wa filamu hiyo ambayo wahusika wake nji wasanii wa hapa nchini, umewezekana kutokana na ufadhili kutoka kampuni kadhaa ikiwemo Selcom.
Mkurugenzi wa Kijiweni Productions, Amil Shivji anasema wamefurahishwa na hatua ya Selcom kuwa mmoja wa wadhamini wa kundi lao.
”Tumefurahi kwamba Selcom wametudhamini. Ni kweli kwamba kampuni nyingi kwenye sekta binafsi wanaogopa kuunga mkono wasanii kwa namna yoyote kwa kuamini kwamba hawanufaiki kupitia udhamini wa Sanaa,” amesema.
Hata hivyo, amebainisha kuwa hayo ni mawazo potofu kwa sababu wanasahau kuwa sanaa inawezesha maisha ya watu wengi nchini.
“Sanaa Inaakisi mwenendo wa maisha ya kila situ. Tangazo ni sanaa, bango ni sanaa na kuna bajeti maalumu ambayo kitengo cha masoko wanapewa kutumia ili kutangaza shughuli zao.
“Ila unakuta mara nyingi hakuna ubunifu hata kidogo. Selcom wamejitokeza kama washupavu kubadilisha hali ya mambo na kukiri kwamba kama kampuni kubwa ni jukumu lao kusaidia kujenga tasnia ya sanaa na kurudisha hadhi ya wasanii ndani ya jamii.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Selcom, Benjamin Mpamo, amesema udhamini huo kwa Kijiweni Productions si wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho kufanywa na kampuni yake.
“Wiki iliyopita tulidhamini kampeni inayolenga kuelimisha na kupanua uelewa wa umma juu ya umuhimu wa kujua njia za kuzuia na kupambana moto majumbani. Katika kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa miaka mitatu, tumeungana na kampuni ya Alaf kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania na taasisi isiyo ya kiserikali ya United Against Crime (UAC).
“Mwaka jana tulikuwa kampuni ya kwanza ya Kitanzania kudhamini shughuli za Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Tunayafanya hayo katika kutimiza wajibu wetu wa kurejesha kwenye jamii kidogo tunachopata kutokana shughuli zetu za biashara.
Kwa miaka mingi sasa tasnia ya filamu imekuwa kapu la kukusanya ajira za vijana katika nyanja mbalimbali zikiwamo uigizaji, utayarishaji filamu, usambazaji kazi za wasanii na hata kuzitangaza.
Lakini pamoja na hayo yote bado tasnia hiyo haifuatiliwi kwa karibu na vyombo husika. Kama ingefuatiliwa vyema bila shaka mambo yangebadilika, walau hivyo ndivyo anavyoona Shivji.
Kijiweni Productions si jina geni ni kampuni iliyoanzishwa  mwaka 2013, filamu yake  ya mwanzo ikiwa katika mtindo wa filamu fupi iitwayo Shoeshine.
Filamu hiyo ilishinda tuzo ya People’s Choice Award katika tamasha la ZIFF mwaka 2013 na iliendelea kushinda tuzo na kushiriki kwenye matamasha ya filamu nyingi duniani.

No comments:

Post a Comment