Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in ametoa wito kwa Marekani ambayo ni mshirika wake, kusaidia kuzuia vita, licha ya kuendelea kuongezeka msuko suko kufuatia vitisho vya kinyuklia vya Korea Kaskazini.
Bwana Moon alimuambia afisa wa cheo cha juu wa jeshi la Marekani kuwa ni lazima kuwe na suluhu la kidiplomasia.
Jenerali Joseph Dunford, alisema kile ambacho Marekani imekipa kipaumbele ni njia za kidiplomasia, akiongeza kuwa Marekani imajitolea kuilinda Korea Kaskazini kutokaka na shambulizi la kijeshi.
Jumatatu Korea Kaskazini ilisema kwa vita vyotote vinaweza kugeuka na kuwa vya kinyuklia.
Pia siku ya Jumatatu wizara ya biashara nchini China ilitoa amri ya kupiga marufuku ununuzi wa bidhaa kutoka Korea Kaskazini, kuambatana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyotangazwa mapema mwezi huu.
Vikwazo hivyo vilitangazwa kujibu majiribio kadha ya makombora ya Korea Kaskazini.
Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Korea Kaskazini kwa kutishia kushambulia himaya ya Marekani ya Guam. Marekani ina wanajeshi 28,000 nchini Korea Kusini.
No comments:
Post a Comment